Magari Yakiwa kwenye Foleni Magari hayo yakiwa katika foleni ndefu kuelekea kwa babu huyo.
Foleni inaendelea.....
Foleni inaendelea.....
Baadhi ya wananchi waliofanikiwa kufika nyumbani kwa Babu huyo, wakiwa katika foleni kwa ajili ya kusubiri kunywa dawa hiyo na kumuona huyo Babu, ambaye sasa amegeuka kuwa moja ya kivutio.
Hii ni sehemu ya foleni ya magari inayokadiliwa kuwa na urefu wa Kilomita kumi, ikielekea Kijiji cha Samange Kata ya Digodigo Wilaya ya Ngorongoro, kwa ajili ya kupatiwa dawa ya jero (500) inayodaiwa kutibu magonjwa matano sugu likiwamo la Ukimwi pamoja na kumuona Babu huyo mwenye miujiza ya ajabu aliyeibuka hivi karibuni. Pamoja na urahisi wa gharama ya kupata dawa hizo laikini bado ni shughuli kubwa kufika katika eneo hilo analoishi Babu huyo kutokana na njia mbaya na umbali mrefu kutoka maeneo ya mji, kwa ujumla Miundombino ya kufika eneo hilo ni mibovu. Kwa mtu kama huyu Serikali sasa ifikie hatua ya kumuangalia kwa jicho la tatu ili kumuwezesha kutoa huduma hiyo kwa ufasaha na ikibidi kuboresha Miundombinu ya Barabara ili wananchi wengi wenyematatizo yanayohusianiana na dawa zake waweze kumfikia kwa urahisi na hata wageni kutoka nje ya nchi waweze pia kufika kwa urahisi. Na pia hata Wizara ya Afya isimamie ipasavyo zozei hilo kutokana na Babu huyo kutoa huduma ambazo hata hospitali ni ngumu kupatikana kwa haraka na pengine hupatikana kwa gharama kubwa tofauti na gharama za babu huyo. Picha hizi ni kwa Hisani ya Blog ya Winde Sizza, Loliondo kupitia Blogspot ya Issamichuzi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)