MAANDAMANO YA CHADEMA CHATO NA KATORO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAANDAMANO YA CHADEMA CHATO NA KATORO


 Wadau Jana nilikuwa kwenye maandamano katika Wilaya ya Chato nyumbani kwa Maghufuli ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Maandamano yalikuwa ni ya Kilometa nane yaliyoshirikisha magari,pikipiki na waendao kwa miguu. Baada ya maandamano kama kawaida ulifanyika mkutano mkubwa wa hadhara. wakati tunarudi Mwanza tukafanya maandamano madogo na mkutano wa hadhara katika Kata ya Katoro jimboni Busanda ambako nako watu walijitokeza kwa wingi. Hakika watanzania wameamua kuunga mkono mabadiliko.

Maandamano Kanda ya Ziwa ndio yamehitimishwa na baadhi ya Viongozi wamesharejea kwenye Makazi Yao.Tumehitimisha kwaajili ya kufanya tathmini na kujipanga upya kwaajili ya Kanda zingine.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.


Kutoka Jijiji Mwanza

Regia E Mtema

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages