KIKWETE AFANYA ZIARA WIZARA YA FEDHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KIKWETE AFANYA ZIARA WIZARA YA FEDHA

Prof. Mkulo akisoma hotuba mbele ya rais kuhusu shughuli zinazofanywa na Wizara yake.


Baadhi ya maafisa wa wizara ya fedha wakimsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete ambaye leo ametembelea wizara hiyo na taasisi zake.
Rais Kikwete akiendelea kusalimiana na maafisa wa wizara ya fedha huku afisa usalama wa taifa akiimarisha ulinzi kwa watu waliotaka kumsogelea bila utaratibu.
Rais Kikwete akiongea na maafisa waandamizi wa wizara ya fedha (hawapo pichani)
Rais Kikwete akitoka nje ya ukumbi wa wizara ya fedha huku Prof. Mkulo akiteta naye jambo.
 
Rais Kikwete akiwaaga maafisa wa wizara ya fedha baada ya ziara yake.

RAIS wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete  leo ameitembelea Wizara ya Fedha kwa mara kwa kwanza kwa mwaka huu na kujioneo maendeleo na shughuli zinazofanywa na  wataalaamu wa wizara  hiyo.

Kabla ya kuitembelea wizara hiyo, Rais Kikwete alifanya ziara Mamlaka ya  Mapato Tanzania (TRA)  na baadaye alikwenda bandarini kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa huko.

Akielezea maendeleo ya wizara yake mbele ya rais, Waziri wa Fedha Prof.  Mustafa Mkulo alisema kwa kiasi kikubwa wizara yake imetekeleza  yote ambayo Rais  Kikwete aliagiza mwaka 2006 alipotembelea wizara hiyo  kwa mara ya kwanza.

Mkulo alisema mpaka sasa wizara yake imefanikiwa kutatua matatizo mengi ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwahisha mishara ya watumishi wa serikali ambapo kwa sasa wanapata mishahara yao tarehe 23 badala ya kusubiri hadi tarehe ya mwisho wa mwezi.
HABARI/PICHA: HARUNI SANCHAWA/GPL

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages