Rais Jakaya Kikwete akihoji jambo kwa Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bi. Agnes Kijazi (aliyesimama) kuhusu utendaji na Utoaji wa Taarifa sahihi za Hali ya hewa Nchini ambapo amesema serikali inaendelea kuboresha na kuijengea uwezo wa vifaa vya kisasa Idara hiyo ili iweze kwenda na wakati na kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Watendaji wa Wizara, Idara, Mamlaka na Taasisi za Wizara ya Uchukuzi Jana jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amewataka viongozi hao kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili wizara hiyo zikiwemo uboreshaji wa huduma za reli, usafiri mijini,uboreshaji wa huduma za bandari, matengenezo ya viwanja vya ndege nchini na migogoro ya wafanyakazi.
Naibu waziri wa Uchukuzi Athuman Mfutakamba (kulia) akizungumza jambo na Rais Jakaya Kikwete katika ukumbi wa wizara ya Uchukuzi Jana jijini Dar es Salaam . Rais Jakaya Kikwete aliitembelea Wizara ya Uchukuzi ili kupata taarifa ya utendaji kazi wa Wizara, Mamlaka, Taasisi na Idara zilizo chini ya wizara hiyo.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akisalimiana kwa furaha na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu( SUMATRA) Bw. Israel Sekirasa mara baada ya kuhitimisha ziara yake Wizara ya Uchukuzi jana jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Eng. Omari Chambo (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)