Mtunzi wa Filamu ya Tears on Valentine Day, Eric James Shigongo akitoa neno katika uzinduzi wa filamu hiyo. Wengine pichani ni baadhi ya washiriki wa filamu hiyo.
FILAMU kali ya Tears on Valentine Day iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa muvi za Kibongo, hatimaye jana ilizinduliwa rasmi kwenye Ofisi za Kampuni ya Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam majira ya usiku.
Katika uzinduzi huo ambao haukuwa na kiingilio chochote, wakazi mbalimbali wa Jijini Dar es Salaam na wanaoishi karibu na kampuni hiyo walifika kwa wingi kuona shughuli pevu iliyooneshwa na wakali wa muziki wa kizazi kipya Steve RnB, Baby Boy, Silver na Hamisi Ramadhan Baba ‘H-Baba’, sambamba na Bendi ya Stone Maiyasika ‘Vijana wa EPA’.
Filamu ya Tears on Valentine Day imetungwa na mtunzi mahiri katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Eric James Shigongo ambaye ni mtunzi wa filamu nyingine kama vile From China With Love na Fake Pastors.
Filamu hiyo yenye kusisimua kila unapoiangalia imeingia mtaani leo Siku ya Wapendanao (Februari 14).

H-Baba akiimba pamoja na mashabiki wake waliohudhuria katika uzinduzi huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)