SPIKA ANNE MAKINDA: SERIKALI TOENI MAELEZO YA KUZAGAA NOTI BANDIA MPYA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SPIKA ANNE MAKINDA: SERIKALI TOENI MAELEZO YA KUZAGAA NOTI BANDIA MPYA


Spika wa Bunge Anne Makinda akifafanua jambo
----
Spika wa Bunge Anne Makinda ameiagiza serikali kutoa maelezo kuhusu tatizo la kuzagaa kwa noti bandia mitaani.Mheshimiwa Spika Anne Makinda ametoa agizo hilo leo bungeni mjini dodoma baada ya mbunge wa jimbo la mji mkongwe Mheshimiwa Mohamed Sanya kumkabidhi noti baandia ya Tsh 10.000 kw amujibu wa maelezo yake bungeni ni kwamba aliipata noti hiyo kutoka kwa mfanyabiashara mdogo aliyemuomba aipeleke bungeni  na kuikabidhi kwa spika na kwamba kiwango cha Elfu kumi ni kipato cha wiki nzima kwa mfanyabishara huyu kijana.

'Benki kuu ya Tanzania ilichapisha noti mpya na kuzisambaza lakini hata kabla ya siku 100 kupita wajanja wachache wa ndani au wa nje wanachapisha noti hizo na hapa dodoma zipo  Mheshimiwa Spika.'

Noti hiyo ya bandia iliyokabidhiwa kwa mheshimiwa spika leo ilikua haina alama ya baba  wa taifa na mbunge huyo ameiomba serikali kuchukua hatua za dharura na za haraka kuwaelewesha wananchi alama mpya za noti mpya.

*Habari hii na Joseph ishengoma -MAELEZO-Dodoma

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages