Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika eneo linalojengwa nyumba ya makazi ya Spika wa Bunge lililoko eneo la Uzunguni Dodoma leo na kupokelewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Bw. Didas Wambura na Mhandisi Philemon Mzee .Jengo hili linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei 2011 Spika Makinda akisaini katika kitabu cha wageni. Spika akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa eneo la Ujenzi (site engineer) Bwana John Thomas. Mfanyakazi mmoja katika eneo la ujenzi akisalimiana na Mama MakindaMwonekano wa jengo kwa nyuma na ujenzi unaendelea.Picha na Prosper Minja
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)