Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,(katikati) Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Rashid Othman (Kulia) wakisoma Dua ya pamoja baada ya Sala ya kusalia Mwili wa Marehemu Ramadhani Said Mkoma mfanyakazi wa Ofisi ya Rais Ikulu aliyefariki Dunia jana kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu Darajani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwafaraji wanafamilia wa Marehemu Mzee Ramadhani Saidi Mkoma aliyekuwa mfanyakazi wa Ofisi ya Rais Ikulu aliyefariki Dunia jana kwa ajali ya gari baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongana na gari aina ya Hiace,ajali hiyo ilitokea eneo la Ruvu Darajani wakati msafara wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ulipokuwa ukielekea Chalinze Mkoa wa Pwani.Picha na Amour Nassor VPO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)