RAISI KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA KIBAIGWA DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAISI KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA KIBAIGWA DODOMA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wafanyabiashara na wananchi katika soko la Mazao la Kibaigwa lililopo wilaya ya Kongwa,mkoani Dodoma leo asubuhi wakati aliposimama kwa muda sokoni hapo kukagua na kujionea hali halisi ya upatikanaji wa mazao na uhifadhi wa mazao sokoni hapo.Mwaka 2006 wakati wa ziara yake katika soko hilo Rais alitoa agizo la kutoanika mazao chini ili kulinda afya ya mlaji.Agizo hili limetekelezwa vyema na sasa mazao yanahifadhiwa vyema kuzingatia kanuni za afya.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mahindi yanayouzwa katika soko la kimataifa la mazao la Kibaigwa wilayani Kongwa,mkoa wa Dodoma leo asubuhi.Kwa mujibu wa uongozi wa soko hilo katika kipindi cha miaka sita kuanzia 2004 hadi 2010 soko hili limeweza kupokea tani za mazao 532,854 na kusafirisha tani 529,143 za mazao tofauti.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages