RAISI JAKAYA KIKWETE ATUA IVORY COAST KWAAJILI YA UPATANISHI WA KISIASA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAISI JAKAYA KIKWETE ATUA IVORY COAST KWAAJILI YA UPATANISHI WA KISIASA

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo muda mfupi baada ya kuwasili jijini Abidjan kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu na mpinzani wa Gbagbo Bwana Allasane Ouatarra. Rais Kikwete yupo katika jopo la kamati maalumu ya Viongozi wa Afrika walioteuliwa na Umoja wa Afrika(AU) kutafuta suluhu ya kisiasa nchini Ivory Coast.Viongozi wengine walio katika kamati hiyo ni pamoja na Rais Jackob Zuma wa Afrika Kusini,Rais Idriss Deby wa Chad,Rais Blaise Compaore wa Burkina Fasso na Mwenyekiti wa kamati hiyo Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.
Marais wanaounda kamati maalumu ya wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Rais Laurent Gbagbo katika ikulu ya Abidjan jana jioni.Kutoka kushoto walioweka vichwa pamoja ni , Rais Idriss Deby wa Chad,Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa kamati hiyo Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.Picha na Freddy Maro-IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages