Mwizi, Phillip Niere, alivyokamatwa na polisi.
MWIZI wa kutumia silaha, Phillip Niere, amewafungulia polisi wa Ujerumani mashitaka kwa kumkamata wakati suruali yake ikiwa imeteremka hadi miguuni.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 alikamatwa baada ya kuwatishia wafanyakazi wa Benki ya Noris huko Aachen, Ujerumani Magharibi, wampe Paundi 200,000 la sivyo angewafanyia “kitu mbaya”.
Mtu huyo alikamatwa baada ya mtoa fedha mmoja kubonyeza kitufe maalum cha dharura bila jambazi huyo kujua.
Polisi waliweza kumpoza kwa kumwambia kwamba iwapo angetulia wasingemletea matatizo yoyote.
Jamaa huyo alisalimu amri baada ya saa moja na kuondolewa kwenye benki hiyo, akapelekwa mtaani suruali yake ikiwa imeteremkia miguuni na jaketi lake likiwa limemfunika usoni.
Niere alisema “alidhalilishwa” baada ya kupitishwa mitaani huku nguo yake ya ndani ikiwa inaonekana.
Mwanasheria wake alisema: “Kufungwa pingu ni kawaida, lakini polisi lazima waeleze kwa nini walimkamata mtu huyo na kuondoka naye wakati suruali yake ikiwa imeangukia miguuni. Huo ni uvunjaji dhahiri wa haki za binadamu.”

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)