MMILIKI WA DOWANS AKAGUA MITAMBO YAKE ILIYOPO UBUNGO TANESCO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MMILIKI WA DOWANS AKAGUA MITAMBO YAKE ILIYOPO UBUNGO TANESCO


Picha Hapo Juu Ni Mmiliki wa Dowans Ambaye alipofanya Kikao Na Wahariri wa Vyombo Vya Habari alikataa kupigwa na kupelekea Wananchi kuwa na shauku ya kutaka kujua ni nani mmiliki Wa Dowans.
Kamera ya Mwananchi Imefanya Kazi ya Kuitafuta na kuipata Sura ya Mmiliki wa Dowans Big Up Mwananchi kwa kukata Kiu ya Wananchi waliokuwa na Shauku ya kutaka kumjua mmiliki wa Dowans.
Mmiliki Wa Dowans mwenye kanzu nyeupe Akikagua Mitambo Yake iliyopo Ubungo.
Gari Aina Ya Land Cruiser Nyeusi kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu Ndio iliyombeba Mmiliki Wa Dowans Suleiman Al Adawi kumpeleka Ubungo kukagua mitambo yake ambayo imeleta utata na kuipelekea Tanesco kuilipa Dowans Fidia ya Sh 94 Bilion mara baada ya kukatisha Mkataba wake na Dowans.
Gari la Mmiliki Wa Dowans Likiwa linaingia ndani ya Eneo la Tanesco lililopokua linampeleka Ubungo kwaajili ya Kukagua Mitambo yake
Walinzi wakilifungulia Gari lililombeba mmiliki wa Dowans Wakati anaingia Kwenye Eneo la Tanesco Ubungo Kwa ajili Ya Kukagua Mitambo Yake.
Mmiliki Wa Dowans Suleiman Al Adawi Akianza Kazi Ya Kukagua Mitambo Yake Iliyopo Eneo la Tanesco Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
Picha Kwa Msaada Wa Michuzi Blogu na Gazeti la Mwananchi.
Kwa Taarifa Zaidi Za Mmiliki Wa Dowans   <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages