MANJI APANDA KIZIMBANI MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MANJI APANDA KIZIMBANI MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JANA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji (kulia) akiongozana na Katibu wake, Mhingo Rweyemamu, wakati wakiingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Jana mchana kwa ajili ya kuwasilisha vielelezo na kutoa ushahidi katika kesi yake dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi. Katika kesi hiyo Manji alimtaka Mengi kumlipa fidia ya Sh 1 tu pamoja na kumuomba radhi kupitia Televisheni yake ya ITV kwa muda wa siku saba mfululizo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji, akizungumza na wakili wake Mabele Marando, wakati alipoingia kwenye Chumba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa ushahidi na kuwasilisha vielelezo vya kesi yake dhidi ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi.
Manji akipitia file lake kabla ya kuingia katika chumba cha Mahakama kuanza kutoa ushahidi.
Akiendelea kuperuzi file lake huku akijipoza kwa fegi.

Vijana wakishusha mzigo wa magazeti yaliyofika Mahakamani hapo katika gari la Tani tatu na nusu kwa ajili ya ushahidi wa kesi hiyo. Miongoni mwa Magazeti hayo ya vyombo vya habari mbalimbali vya nchini mengi ni yale yaliyokuwa yakichapisha habari za kawaida zisizomchafua Manji tangu mwaka 2006 hadi 2011 machache ni yale yaliyokuwa yakichapisha habari zinazomchafua Manji kwa kipindi kama hicho cha tangu 2006 hadi 2011.
Vijana wakishusha TV katika gari hilo kwa ajili ya kuonyeshea ushahidi Mahakamani hapo.
Kwa Hisani Ya SUFIANI MAFOTO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages