NOTI MPYA ZATIKISA BOT - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NOTI MPYA ZATIKISA BOT

 Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania Prof BENNO NDULU alipokuwa Akitoa Ufafanuzi Juu Ya Ubora Wa Noti Mpya Wakati Wa Kikao Na Waandishi Wa Habari Hapo Jana Dar Es Salaam.
 Picha ya Noti Mpya Ya Rwanda, Marekani na Noti Mpya ya Tanzania na Noti Ya zamani Ya Tanzania
 Mkurugenzi Wa Kampuni Ya Crane Curreny Bwana Peter Brown Akichubua Rangi Ya Noti Mpya
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imelazimika kumleta nchini, Mkurugenzi wa Kampuni ya Crane Curreny, ya Sweden iliyoshinda zabuni ya kutengeza noti mpya zilizoanza kutumika Januari mwaka huu, kueleza ubora wake baada ya noti hizo kuhisiwa kuwa zinachuja na ni rahisi kughushiwa.Ujio wa mtaalamu huyo, Peter Brown ni utekelezaji wa ahadi ya Gavana wa BoT, Professa Benno Ndullu aliyoitoa wiki mbili zilizopita kuhusu taasisi yake kufuatilia ubora wa noti mpya ambao ulianza kutiliwa mashaka na baadhi ya wananchi.

Januari 23, mwaka huu gazeti hili liliripoti habari ya uchunguzi iliyoelezea mashaka kuhusu ubora wa noti hizo mpya, baada ya kubainika kuwa baadhi zinachuja na kuacha rangi zikilowa maji au jasho.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, noti hizo hasa za Sh5,000 na Sh10,000 pia zilibainika kuwa zikikandamizwa kwenye karatasi nyeupe bila kulowanishwa na maji au jasho, huacha rangi.
Kwa taarifa zaidi  <<<<<< BOFYA HAPA >>>>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages