KLABU YA SIMBA YAGOMEA MECHI ZA KIMATAIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KLABU YA SIMBA YAGOMEA MECHI ZA KIMATAIFA

 
Na Khadija Mngwai
KLABU ya Simba imesema baada ya suluhu dhidi ya Elan Club Mitsoudje ya Comoro haitocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na badala yake itatumia Ligi Kuu ya Bara kuwaua wapinzani wao hao katika mechi ya marudiano.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema, uongozi umejipanga vema kuhakikisha timu inafanya vizuri kwenye mchezo huo kupitia mechi ya Afrika Lyon inayonolewa na Jumanne Charles (iliyocheza nao jana) na Tanzania Polisi iliyo chini ya John Simkoko.

“Muda ni mdogo kuweza kutafuta timu za kujipima, tunaamini Lyon na Polisi Dodoma, ndizo zitakazotumika kuandaa kikosi,” alisema Mtawala.

“Upande wa uongozi uko safi kwa kuandaa mazingira mazuri kuhakikisha timu inafanya vizuri hapa nyumbani na kufanikiwa kusonga mbele,” alisema Mtawala.

Simba itarudiana na Wacomoro hao katika Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Februari 11 mpaka 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo mshidi wa hapo ataikabili TP Mazembe ya DR Congo katika hatua inayofuata.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages