Baadhi ya askari wa jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao hawajaoa wanaoishi katika Kambi ya KJ 511 Gongolamboto, walioathirika na mabomu, wakiwa katika eneo la hafla ya kukabidhiwa msaada wa Robota la Mitumba na Soda za Sippy. Msaada huo ulitolewa na Kampuni ya Super Sippy Ltd, iliyokabidhi msaada kwa askari hao pamoja na kwa wananchi waliopatwa na matatizo hayo, ambapo jumla ya msaada huo ulikuwa ni Sh. milioni tatu.Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wanaoishi katika Kambi ya 511KJ Gongolamboto jijini Dar es Salaam (makapera), wakibeba robota la mitumba na soda za Sippy, walizokabidhiwa na Kampuni ya Super Sippy Ltd, waliofika kambini hapo Jana mchana na kutoa msaada huo wa nguo na soda.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Super Sippy, Mussa Kisia, akimkabidhi msaada wa Robota la Mitumba, askari wa kike Fadhila Suleiman, kwa niaba ya askari wenzake makapela wasiooa na wasioolewa, walioathirika na mabomu yaliyolipuka katika kambi yao wanayoishi ya KJ 511 Gongolamboto hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa Kambi hiyo, Kanal Aloyce Mwanjile.
Mkuu wa Kambi hiyo, Kanal Aloyce Mwanjile, akizungumza na askari hao wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa msaada huo jana mchana.
Meneja Mauzo wa kampuni ya Super Sippy Limited, Mussa Kisia (kushoto) akimkabidhi msaada wa Marobota mawili na soda za Sippy, Katibu Tawala msaidizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Eliya Ntandu, kwa niaba ya wananchi walioathirika na mabomu wakati kampuni hiyo ilipofika Gongolamboto leo mchana kukabidhi msaada huo wenye tahamani ya Sh. milioni 3.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)