'MAANDALIZI YA KOMBE KA KAMANDA KOVA'Kamanda Kova (wapili kulia), Rais wa Kampuni ya mafuta ya RBP Oil, Rahma Al-Kharoos (katikati), Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dokey (kulia) na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela (kushoto) wakiongoza maandamano ya matembezi ya hiyari yaliyoanzia Makao Makuu ya Polisi Centre hadi kwenye viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa Road, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Kova yanayotarajia kuanza Machi 12 jijini Dar es Salaam na kuzishirikisha timu mbalimbali za kiraia, Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ) yatakayofanyika katika viwanja vitatu tofauti vya jijini.
Wengine katika maatembezi hayo hawakujua umuhimu wala maana ya matembezo hayo 'Joging', kwani badhi yao walionekana kutinga Majinzi na viatu vya mtoko kama mdada huyu anavyoonekana hukuwenzake wote wakiwa na mavazi ya kimichezo.
Eeeeh! Safari inaendelea Taratiiiiibu wanasonga....
Kama hawatembei vile kumbe taratibu wanamaliza......
Othmani Kazi akiwaongoza Makamanda kufanya mazoezi ya kukimbia katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa Road leo asubuhi baada ya kumaliza matembezi hayo ya Joging.
Baadhi ya maafande na raia walioshiriki matembezi hayo.
Baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa Road kila mmoja alijaribu kuonyesha umahiri wake wa kufanya mazoezi ayawezayo, huyu ni mmoja wa Makamanda akitimua mbio katikati ya uwanja kuwawahi kina Kamanda Kova waliokuwa tayari wameanza mazoezi ya kukimbia, weee palikuwa patamu hapo jinsi alivyokuwa akipiga hatua kutimua mbio weee acha tuuuuu.
"Wengine tumezoea mazozi ya kucheza sebene bwana wacha tujimwage"
Wengine japo walikuwa wakifanya mazoezi kwa kufuata biti za muziki lakini walikuwa watunga sheria jinsi ya kuanza kusakata rhumba wakati wenzao wanaendele na mazoezi, Hawa ni miongoni mwa walioshindwa kuvumilia na kuamua kukacha mazoezi na kusonga mbele ya wenzao na kuanza kulisakata rhumba.
Kamanda Kova (kushoto) akimalizia mbio kwa spidi kali ili kuwashinda Makamanda wenzake wakati wa mazoezi hayo leo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)