HOTELI YA NEW AVON KUIDHAMINI TASWA FC - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HOTELI YA NEW AVON KUIDHAMINI TASWA FC



HOTEL mpya kabisa ya kisasa, New Avon Hotel imetangaza kuidhamini Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC .
Mkurugenzi Mtendaji wa New Avon Shaheed Dhanani alisema kuwa wanatambua mchango mkubwa wa timu hiyo katika maendeleo ya soka na michezo nchini.
Shaheed alisema kuwa kwa vile wanaingia rasmi katika biashara ya hotel na kutokana na ubora wa hotel yao, wameamua kuisapoti timu hiyo na wanaamini watafanya vyema kupitia udhamini wao.
“New Avon Hotel itatoa jezi zenye thamani ya dola za kimarekani 900 ambazo kwa sasa zinachapishwa huko Dubai, ni jezi za kisasa na zina ubora wa hali ya juu,” alisema Shaheed.
Alisema kuwa mbali ya jezi, pia watatoa soksi kwa wachezaji ili waonekane smati kama ilivyo hotel yao ambayo ipo katika makutano ya mitaa ya Aggrey na Jamhuri (Mnazi Mmoja).
Alisema kuwa wanatarajia kuongoza katika soko la hotel nchini kutokana na huduma zao na ubora wa hotel hiyo na ndiyo maana wameamua kuidhamini Taswa Fc ikiwa ni timu bora ambao tokea kuanza kwa mwaka huu haijafungwa.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza New Avon Hotel na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika kuinadi hotel hiyo katika mechi na shughuli zake.
“Tunajivunia kuwa na New Avon Hotel, tunakubali msaada wao na tunahaidi kufanya vyema katika mechi zetu kupitia msaada wa hotel hiyo, ” alisema Majuto.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages