HARAMBEE YA GONGO LA MBOTO READING YAFANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HARAMBEE YA GONGO LA MBOTO READING YAFANA

 
Wadau wa Harambee; kutoka kushoto J J, Chisumo, Miss Jestina, Gardol na Frank
 
Frank kutoka Urban Pulse  akiwa na Tina kutoka Miss Jestina Blog baada ya harambee
 
'Toa ndugu' ikiendela
Mtoto Chanele akimpa mchango wake Miss Jestina
Salam,
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Watanzania wote  waishio  Reading UK walioweza kuja Leo mchana Vincent  kuchangia wahangwa wa Gongo la Mboto  Tanzania. Kwa mda wa saa moja tumekusanya Jumla ya  pesa taslim Pounds £200.  Pia tumekusanya nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali. Tafadhali Kumbuka bado hujachelewa kwa wakazi wa Reading ambao hawakuweza kufika leo mnaweza kupeleka michango yenu Vincent siku ya mwisho ya kukusanya ni Jumanne ijayo tarehe 1.3.11.

Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE, MISS JESTINA BLOG, AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, MRS NASIBU NA Utawala wa Vincent Restaurant Reading kwa kusaidia zoezi la leo.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages