DKT JOHN POMBE MAGUFULI: NITABOMOA HATA MAJENGO YA CCM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DKT JOHN POMBE MAGUFULI: NITABOMOA HATA MAJENGO YA CCM

*ASEMA TANESCO, WIZARA YA MAJI WAMEKALIA NAO KUTI KAVU
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli (pichani) ametangaza msimamo wake mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kusema, "nitabomoa nyumba zote zilizomo kwenye hifadhi ya barabara hata kama ni mali ya CCM, kwani nimekula kiapo cha utiifu kusimamia sheria za nchi."

Kadhalika, Dk Magufuli amesema ofizi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), na Makao Mkuu ya Wizara ya Maji, nazo zipo katika hifadhi ya barabara na kwamba ikiwa kutakuwa na mpango wa upanuzi wa barabara ya Morogoro, nazo zitalazimika kubomolewa kwa mujibu wa sheria.

Dk Magufuli ameshaanza kutekeleza msimamo wake huo baada ya kuagiza ubomoaji wa Ofisi ya Wakala wa Barabara (Tanroads), Mkoa wa Dar es Salaam ambayo iko chini ya wizara yake.

Ofisi hiyo iliyokuwa imejengwa katika eneo la Kituo cha Mabasi ya Abiria Ubungo jijini Dar es Salaam tayari imekwishabomolewa. 

Akizungumza wakati na baada ya kikao kati ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Wizara na wadau mbalimbali ikiwamo Polisi na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk Magufuli alisema hata ofisi ya Tanesco na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, zimo ndani ya hifadhi ya barabara.
Kwa Stori Zaidi  <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages