BAADA ya malumbano, mijadala mbalimbali kuhusu Katiba Mpya ya nchi na Rais Jakaya Kikwete kuridhia kuwa nayo, wasomi nchini wamejipanga kutoa mchango wao.
Hatua hiyo imetokana na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), kuandaa makongamano endelevu ya kujadili mchakato wa Katiba hiyo.
Kwa mujibu wa Udasa, makongamano hayo yatafanyika kwa mwaka mzima ambapo pamoja na mambo mengine, haja na maudhui ya Katiba iliyopo na mpya vitajadiliwa kwa kina.
Katika Kongamano la kwanza litakalofanyika Januari 15 kuanzia saa nne asubuhi pamoja na mambo hayo, pia ubaya na uzuri wa kuundwa Tume ya kushughulikia uratibu wa Katiba vitajadiliwa.
Suala la uundwaji wa Tume alilisema Rais Kikwete alipotoa hotuba yake ya salamu za Mwaka Mpya mwishoni mwa mwaka jana, ambapo aliridhia mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na kueleza kuwa ataunda Tume kufanikisha hilo.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana chuoni hapo, viongozi wa Udasa akiwamo Mwenyekiti wake, Dk Mashumbusi Kabogoya, Makamu Mwenyekiti, Dk Kitila Mkumbo na mwakilishi wa wanajumuiya hiyo, Dk Azaveli Lwaitama, walisema kongamano hilo linatarajiwa kutoa mwongozo wa namna nzuri ya upatikanaji wa Katiba mpya.
Akijibu maswali ya waandishi waliotaka kujua kama kongamano hilo halina mwelekeo wa kumwingilia Rais katika utekelezaji wake wa kuunda Tume Huru ya kushughulikia mchakato wa Katiba, Dk Kabogoya alisema,“ tutazungumzia ubaya na uzuri wa Tume, hatumwingilii Rais kwa namna yoyote, maana sisi tutazungumza kitaaluma, na sidhani kama Rais atawaza hilo kwa namna ninavyomfahamu.”
Akifafanua zaidi, Mratibu wa Kongamano hilo, Dk Mkumbo alisema, “hata hivyo Tume
ikiteuliwa na mtu mmoja, si Tume shirikishi hiyo, kwa kuwa itapaswa kuwajibika kwa aliyeiteua, Tume shirikishi inateuliwa kwa kushirikisha.”
Dk Mkumbo bila kubainisha tume hizo, alisema nchi hii ina historia ya tume nyingi zilizoundwa kwa kazi maalumu kama hiyo, lakini mwisho wa kazi walipaswa kuwajibika kwa aliyewatuma na si kwa wananchi kama inavyopaswa kufanya Tume shirikishi.
Katika hilo, alisema ndiyo sababu ya kuwapo kongamano hilo ambalo ni ufunguzi wa makongamano endelevu kama hayo, ya kuchambua kwa pamoja, haja ya Katiba mpya, maudhui, ubaya na uzuri wa Tume na kuhadharisha kuwa jukwaa hilo halitakuwa na mwekeleo wa kutetea chama chochote cha siasa.
Kwa mujibu wa Dk Kabogoya, mwaliko umetolewa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Katiba na Sheria, vyama vya siasa na vya kiraia na wananchi wa kawaida wenye nia ya kujifunza na si ushabiki wa siasa.
Dk Kabogoya aliongeza kuwa watakaowasilisha mada katika kongamano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah ni Profesa Issa Shivji na Jenerali Ulimwengu.
Alisema wana mpango wa kurejesha hadhi ya chuo hicho ambacho zamani kilikuwa na makongamano ya kuibua mijadala yaliyokuwa yakihudhuriwa hata na Rais Julius Nyerere, lakini baadaye yalitoweka.
Awali akielezea mantiki ya kongamano hilo, Dk Kabogoya alisema lengo ni kutoa fursa kwa wananchi kufahamu misingi ya jumla ya Katiba ya sasa, kupendekeza njia bora itakayotumika katika mchakato wa uundwaji Katiba mpya ili kuepuka malalamiko na Katiba isiyo na viwango.
“Hatuji Jumamosi kutengeneza Katiba mpya, watu wajue hilo mapema, hatuna uwezo huo, ila Katiba yetu ya Udasa imetupa nafasi ya kuibua na kuhamasisha masuala ya kitaaluma, tusipokuwa makini katika hili, tutakuwa na Katiba mbovu kuliko inavyodhaniwa,” alisema Dk
Kabogoya.
Mwenyekiti huyo wa Udasa alitumia pia fursa hiyo, kubainisha msimamo wa jumuiya hiyo kuhusu Katiba mpya kwa kusema msimamo wao ni Katiba mpya na kuongeza: “Kila mwananchi anahitaji hilo sasa, sisi tutakuwa wa ajabu tukilikataa.”
Lwaitama, alisisitiza kuwa, mustakabali wa Taifa hili uko mikononi mwa wananchi hivyo kuwataka wenye nia ya kufahamu Katiba iliyopo na umuhimu wa mpya kama upo, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kongamano hilo.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)