Raisi Wa Zanzibar Akimkabidhi Kombe Nico Nyagawa |
Jackson Odoyo, Unguja
SIMBA imetumia siku 88 kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu kwa kuichapa timu hiyo mabao 2-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Itakumbukwa, Yanga iliifunga Simba bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Oktoba 16, mwaka jana na alikuwa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete aliyewanyamazisha mashabiki wa Simba waliojazana kwenye uwanja huo wakati imba ilipokuwa ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani baada ya Uwanja wa Uhuru kufungwa.
Hata hivyo, katika mchezo wa jana, timu zote ziliwakosa wachezaji wao kadhaa waliokuwa timu ya taifa iliyoko huko Misri kushiriki michuano ya Bonde la Mto Nile ambako timu hiyo ya Tanzania imeshatolewa.
Simba ndiyo iliyoonyesha uchu wa ushindi, ilianza kwa kufanya mashambulizi ya mfululizo langoni mwa Yanga ikiongozwa na Mussa Hassan Mgosi, Haruna Shamte, Nico Nyagawa na Hilary Echessa lakini hata hivyo mashambulizi yao hayakuwa na malengo.
Simba wakicheza pasi za uhakika, walipata bao lao kupitia kwa Mussa Mgosi katika dakika ya 32, baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Yanga. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Yanga ikiongozwa na Davis Mwape katika kutengeneza mashambulizi, ilikianza kipindi cha pili, kujaribu kushambulia, lakini hata hivyo ngome ya Simba ilisimama imara.
Simba ilimtoa Hilary Echesa na nafasi yake kuchukuliwa na Shija Mkina aliyeipatia Simba bao la ushindi na kuzima ndoto za kocha wa Yanga, Kosta Papic kushinda mechi mbili mfululizo.
Hii ni mara ya pili kwa Simba kutwaa ubingwa, itakumbukwa ilitwaa ubingwa huo wa Mapinduzi mwaka 2008.
Pia hii ni mara ya pili kwa Simba kuifunga Yanga kwenye uwanja huo katika mechi ya fainali, kwani 1992, Simba iliifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti baada ya sare 1-1 katika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

Hekaheka Uwanjani Hapo......
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)