MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUAGA MIILI YA MAREHEMU WALIPOTEZA MAISHA KATIKA MAANDAMANO ARUSHA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUAGA MIILI YA MAREHEMU WALIPOTEZA MAISHA KATIKA MAANDAMANO ARUSHA LEO


 
Pichani juu na chini Wafuasi wa Chadema wakiwa wamebeba majeneza ya vijana wawili waliouwawa na polisi mkoani Arusha mapema wiki hii. Ibada ya kuwaombea marehemu ilifanyika katika uwanja wa NMC leo na kuhuduriwa na maelfu ya wakazi wa jiji hilo.
 Wafuasi wa Chadema Wakiwa Katika Maandamano Wakati wanatoka Hospitali Kuchukua Miili Ya Marehemu Na Kuipelekea Katika Viwanja Vya NMC kwa ajili ya Kuaga Miili Hiyo
Wafuasi Wa Chadema Walipokua Kwenye Msafara Kuelekea Viwanja Vya NMCArusha
Mwenyekiti wa Chadema, freeman Mbowe (kushoto) akiongoza ubebaji wa majeneza hayo.
 
Mbowe akiwataka wafuasi wake kuwa watulivu katika ibada hiyo
 
Mke wa marehemu,Ismail Omary akilia kwa uchungu nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru Arusha wakati wa kuelekea katika ibada ya kuwaaga marehemu hao.
Ibada imeisha kwenye saa kumi na nusu jioni hii na wengi wameendelea kwenda kuzika USA River anakoishi mmoja wa marehemu(Ndg yetu Marehemu Ismail) na Rombo anakotokea ndg yetu marehemu Denis Shirima. Viongozi wote wa juu waCHADEMA (Mbowe,Dr Slaa, Mzee Ndesamburo, Baadhi ya Wabunge akiwemo Tundu  Lissu,John Mnyika, Halima Mdee, Mustafa Akunay,  na wale wa kuteuliwa  walikuwemo. Naibu meya wa Mwanza,Aliyekuwa naibu meya feki wa Arusha Ndg  Michael Kivuyo naye alikuwepo kutubu nk.Habari hii na Mdau Yona F Maro/ Arusha Wanabidii

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages