NYUMBA ZA KWETU KARAGWE KIJIJI CHA MAKUMBUSHO-KIJITONYAMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NYUMBA ZA KWETU KARAGWE KIJIJI CHA MAKUMBUSHO-KIJITONYAMA



Hii ni nyumba ya kiasili ya Kabila la Wanyambo ambao ni wenyeji wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera.Nyumba hii imejengwa kwa michango ya Wanyambo waishio jijini Dar es Salaam, ndani ya Kijiji cha Makumbusho,Kijitonyama kwaajili ya matumuzi ya kudumisha mila na desturi la Kabila hilo ambalo Ijumaa ya Januari 21 mwaka 2011, inafanya tamasha la kabila letu la Wanyambo.Picha na Happiness Katabazi
--
WENYEJI wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera ambao ni Wanyambo,leo wanatarajiwa kuanza tamasha la siku tatu la kuenzi utamaduni wao ikiwa ni katika kunadi mila na desturi zao.
Asili ya jina la kabila hilo limetokana na maana kuwa Mnyambo ni mtu mwenye asili ya eneo la Maziwa Makuu.Pia asili ya jina la kabila hilo limetokana na aina moja wapo ya ndizi inayofahamika kwa jina la Enyambo.

Aidha neno nyambo linamaanisha mtu au kitu au mmea asilia pia yupo ng’ombe wa asili wilayani Karagwe ambaye anajulikana kwa jina la Enyambo linalofahamika katika nchi za Uganda na Rwanda

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages