Katibu wa Baraza la Sanaa Tanzania, Ghonche Materego (katikati), akipiga makofi mara baada ya kuzindua shulighuli hiyo.
Tamasha la utoaji tuzo Bongo la Kili Music Awards usiku wa kuamkia leo limezinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Double Tree Masaki jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limezinduliwa na Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania, Ghonche Materego, ambapo wasanii na wadau kibao walihudhuria. Tunzo zinatarajiwa kutolewa Machi 26 mwaka huu. Cheki picha za wadau waliohudhuria.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho wa pili (kulia), akiwa kwenye pozi na baadhi ya wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Mwimbaji wa African Stars International, Charles Gabriel ‘Chalz Baba (kulia), akikandamiza kilaji na rafiki yake kipenzi, Ahmed Hashim ‘Petit Man’
Mtangazaji wa Star TV Sauda Mwilima (kushoto), akiwa na DJ Venture (katikati), na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo.
Chidy Benzi (kulia), akibadilishana mawazo na Stara Thomas.
Mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions, Tippo Athumani, (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars Intenational ‘Twanga Pepeta” Asha Baraka na Meneja Mkuu wa GPL, Abdallah Mrisho (katikati). Kulia ni msanii anayejulikana kwa jina la Steve R&B.
Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ (wa pili kushoto), akiwa kwenye pozi na wasanii wenzake, Dogo Janja na Mheshimiwa Temba.
Picha: Musa Mateja/GPL
Picha: Musa Mateja/GPL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)