Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akimlaki Balozi wa Indonesia nchini Balozi Yudhistiranto Sungadi Wizarani.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe katika mazungumzo na Balozi Yudhistiranto Sungadi Wizarani.
Na. Alpha Natai na Issa Sabuni, WKCU
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Indonesia nchini Balozi Yudhistiranto Sungadi Wizarani. walizungumzia kuhusu uwezekano wa Indonesia kushirikia na Tanzania kwa kuleta wataalam wa masuala ya umwagiliaji ili waweze kutoa mafunzo na elimu wakishirikiana na wenzao wa hapa nchini katika kufanikisha Kilimo cha umwagiliaji.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amefanya mkutano mdogo na Barozi Sungadi ofisini kwake jana katika mkutano huo mfupi Waziri Meghembe alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi Sungadi wa Indonesia kwa ushirikiano mkubwa uliopo baina ya nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali hasusan Kilimo.
Mhe. Prof. Maghembe vilevile alichukua fursa hiyo kuialika Indonesia kupitia Balozi wake nchinii kushiriki maonesho ya kimataifa ya biashara ya Saba Saba na yale ya kitaifa ya Kilimo, Nane Nane ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Julai na Agosti.
Katika baadhi ya mambo yaliyozungumzwa ni pamoja na Waziri Maghembe kushukuru kwa mfumo wa Shamba Darasa ambapo kwa asili ulitokea Indonesia ukijulikana kama Farmer Field School, misaada ya mashine rahisi za kilimo hususan zile za kupandia mpunga na ujenzi wa Chuo cha Mafunzo kwa Wakulima cha Masonga (Masonga Farmers Training).
Kwa Msaada Wa Michuzi Blog.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)