NI kwa mara nyingine tena miamba miwili ya soka nchini, Simba SC na Yanga SC zinakutana kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar, katika fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi. Mechi ambayo itapigwa majira ya saa 10 jioni. Roho za mashabiki zipo juu juu kutokana na mpambano huo kwani hamna mtu ajuaye nani ataibuka kidedea hapo kesho.
Simba itakuwa ikimtegemea zaidi mshambuliaji wake Mganda Emmanuel Okwi wakati Yanga itakuwa na matumaini kupitia nyota wake mpya Mzambia Davies Mwape. Hakuna cha sare, hapo lazima mmoja aondoke kichwa chini huku mwingine akishangilia.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)