Baadhi ya wahitimu wa digrii ya Udaktari wa Afya ya Meno(Doctor of Dental Surgery) wakila kiapo cha uaminifu na utii wa miiko ya udaktari wakati wa Mahafali ya nne ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi,Muhimbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana mchana
Rais Jakaya Kikwete akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Afya ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Mkuu wa chuo hicho, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) wakati wa Mahafali ya nne ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam Jana. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (kulia) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Deogratius Ntukamazina. (Picha na Fadhili Akida)
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi,Muhimbili Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akimtunukia Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Afya ya Jamii(Doctor of Public Health,Honoris Causa) wakati wa mahafali ya nne ya Chuo hicho iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.Kushoto akiangalia ni Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Kisali Pallangyo.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi,Muhimbili Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtunuku Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Afya ya Jamii(Doctor of Public Health,Honoris Causa) wakati wa mahafali ya nne ya Chuo hicho iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.Picha na Fadhili Akida na Freddy Maro/IKULU







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)