Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, akitoa rambirambi za Serikali wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Dk Remmy Ongala aliyefariki majuzi na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Sinza jijini Dar. Shughuli ya kutoa heshima za mwisho ilifanyika uwanja wa Biafra, Kinondoni
Dk. Emmanuel Nchimbi akiongoza umati wa waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa Dk. Remmy Ongala uwanja wa Biafra Kinondoni leo. Kulia ni mtoto mkubwa wa Dk. Remmy, Kalimangonga Ongala ambaye ni mwanasoka nyota.
Mbunge wa Ubungo, Mh. John Mnyika na Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan wakititoa heshima zao za mwisho kwa Dk. Remmy Ongala
Mshirika wa karibu wa siku nyingi wa Dk. Remmy Ongala, Cosmas Thobias Chidumule, akiwa na uchungu wakati wa heshima za mwisho kwa besti wake waliefanya kazi kwa miaka mingi kabla ya wote kuokoka na kuanza kumwimbia Mungu
Toka shoto ni wakongwe Mzee Makassy, Tchimanga Kalala Assosa (wa tatu waliosimama) akifuatiwa na King Kikii, Kanku Kelly na Abou Semhando 
Kwa Hisani Ya Michuzi Blog



















No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)