WANAFUNZI WA VYUO VYA IFM NA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU MOROGOR WAANDAMANA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANAFUNZI WA VYUO VYA IFM NA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU MOROGOR WAANDAMANA LEO

aadhi ya wanafunzi wa Vyuo vikuu vya IFM na Chuo cha Kiislam Morogoro, wakihamaki wakati walipokuwa nje ya Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Msasani jijiji Dar es Salaam leo, walipofika kuulalamikia uongozi wa bodi hiyo kwa kutosimamia taratibu za ulipaji wa ada za wanafunzi na kupanda kiholela kwa ada kutoka Sh. milioni 1 hadi milioni 1.7, jambo linalowafanya baadhi ya wananfunzi kushindwa kulipa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Machunda Lubambula. akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha IFM, wakati akitoa majibu kuhusu malalamiko yao, wakati walipofika kwenye ofisi hizo Msasani jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi hao wakiondoka eneo hili baada ya kutofikia muafaka na kuanza safari ya kuelekea Ofisini kwa Waziri wa Elimu
Kwa Hisani Ya Michuzi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages