Kuna mambo muhimu ya kujifunza kuhusu furaha yako na amani ya mwenzi wako. Labda kabla sijaenda mbele zaidi, nikufafanulie hili: Sanaa ya busara katika maisha inajumuisha vitu vinne.
Navyo ni nia na malengo, Mungu ana nafasi yake, hatua chanya na mafanikio endelevu. Ukikaribisha busara kama kanuni yako ya kuishi, maana yake unahitaji amani na furaha. Hilo liweke akilini halafu tuendelee.
Ukitaka kuishi kwa busara ni lazima uwe na mtazamo wenye furaha. Hii ni shule ndugu yangu, unapaswa kuiangalia dunia kwa fikra na macho. FURAHA; Hebu angalia wengine wanavyosononeka kwa kuikosa, kisha jifunze pia kwa wenye amani.
Mtu sahihi ni yule anayejifunza kupunguza msongo wa mawazo, anayejitahidi kuongeza furaha na kupanua uwezo wake. Kama ndivyo, basi nawe unatakiwa ujiulize:
“Utapata vipi furaha ikiwa mwenzio amenuna?”
Akiwa amekasirika utaweza kucheka? Jibu ni kwamba haiwezekani na endapo moyo wako una amani wakati mwenzako amejikunja, ni wazi kwamba penzi lenu limejaa mashaka. Je, mtaenda hivyo mpaka lini?
Ni vizuri kila mtu ajifunze kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza furaha. Ukifanikiwa kuiweka chanya furaha ya mwenzi wako na yako itapatikana. Zingatia msemo kuwa ninyi ni kitu kimoja, wewe ni yeye!
Watu wengi wamekuwa wakishindwa kustawisha uhusiano wao kwasababu wanashindwa kuishi ndani ya wenzao. Wanatenda mambo ambayo yanawaumiza wenzi wao bila kujiuliza. Hawana malengo chanya!
Mtu mwenye malengo mazuri katika mapenzi ni yule ambaye anajiuliza kabla ya kuzungumza au kutenda. Anatafakari kauli au kitendo na matokeo yake. Pointi kuu ni mapokeo ya mwenzi wake. Ni kosa kufanya tukio lolote au kutoa matamshi yanayoweza kumuudhi mwenzako.
Ni lazima uwe na angalizo kwamba kwako linaweza kuwa dogo lakini kwa mwenzako ni kubwa. Heshimu kosa lolote kwamba linaweza kuhatarisha uhusiano wako, kwahiyo jichunge kila eneo.
Wewe ni mtu hapa duniani, inawezekana uzito wako ni mdogo. Ukiwepo na usiwepo taifa halisomi upungufu wowote! Hata hivyo, kupitia mapenzi wewe ni dunia mbele ya mwenzio. Kila kitu hakina thamani kwake bila uwepo wako, kwahiyo heshimu hisia zake, ingia gharama kumletea furaha.
Mfumo sahihi wa mapenzi ni kuishi ndani ya mwenzako. Kuzijulia hisia zake na kujenga nidhamu ya kuepuka kumpa maumivu yasiyo na sababu. Unaelewa kuwa mwenzako hapendi uchelewe kurudi nyumbani, kwahiyo usifanye makusudi mitaani.

Kwa Story Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)