Pichani ni Marehemu Abubakar Mtamike enzi wa uhai wake
---------
Habari hii na Francis GodwinDiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) Abubakari Mtamike wa kata ya Gangilonga mjini Iringa amefariki dunia gahfla asubuhi ya jana akiwa nyumbani kwake.
Marehemu Mtamike juzi alishiriki vizuri sherehe za kuapishwa kwa madiwani pamoja na kumpigia kura meya wa Manispaa ya Iringa na naibu wake na kuomba kurudi nyumbani kwake baada ya kuanza kujisikia vibaya na majira ya saa 11 alfajiri hali ilianza kuwa mbaya na kufariki dunia.Huyu ni diwani wa pili kufariki dunia ambapo diwani mwingine ni Fatuma Kihombo wa viti maalum kanda ya Ruaha ambaye alifariki mara baada ya kushinda uchaguzi akingoja kuapishwa.
Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Gervas Ndaki ameelezea kwa masikitiko makubwa kifo cha diwani huyo.Mwili wa marehemu unatarajikusafirisha leo kwenda kijijini Kwake Mdandu wilayani Njombe kwa mazishi yatakayofanyika kesho jumapili .
Mtandao huu unaungana na familia ya marehemu na madiwani wote pamoja na wakazi wa kata ya Gangilonga katika maombolezo ya kifo cha diwani Mtamike

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)