MLINZI WA MBUNGE WA MVOMELO AMOS MAKALA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MLINZI WA MBUNGE WA MVOMELO AMOS MAKALA


KATIKA kuonyesha kwamba hana ubaguzi wa aina yoyote katika jamii, Mbunge wa jimbo la Mvomero mkoani  Morogoro Amos Makalla,ameamua kumuajiri  kijana mmoja mfupi ‘Emoro’ anayekwenda kwa jina la Michael Nchimbi, kuwa mlinzi wa nyumba yake iliyopo maeneo ya Kihonda mkoa hapa.

Juzi mtandao huu ulitembelea nyumbani kwa mheshimiwa huyo na kukuta baadhi ya watu wakimshangaa mlinzi huyo aliyekuwa na silaha ya kirungu.

Akizungumza na Mwandishi wetu emoro huyo, Nchimbi (43) alidai kwamba anamshukuru Makalla kwa kumpa ajira hiyo.

“Kwa ulema huu ni vigumu kwa watu wengine kuniamini na kunipa jukumu la ulinzi, kipekee namshukuru mheshimiwa Makalla kwa kunipa ajira hii, pia na toa wito wa watu wengine kuiga mfano  huu kwa mbunge wa Mvomero,” alisema Nchimbi.


Hapa akimpigia saluti ikiwa ni ishara ya salam ya heshima kwa bosi wake.


Hapa akifungua geti.


Akizungumza na bosi wake.


Hapa ni baadhi ya majirani na Makalla wakiomba kupiga picha na Nchimbi.

PICHA ZOTE NA DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages