Kilimanjaro Stars kabla ya gemu
Timu ya taifa ya Burundi
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars,Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka beki wa timu ya Burundi,Nzeyimana Hussein katika mchezo uliopigwa jana ndani ya dimba la Taifa.Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kuikandamiza Burundi mabao 2-0.Nurdin Bakari (mfungaji wa magoli mawili ya kili stars) akijiandaa kuachia shuti kali ambalo ilikuwa almanusra kupachika bao la tatu.
Mshike mshike katika lango la timu ya Burundi ambapo golikipa wake,Niyonkuru Vladimir aliweza kuizuia hatari hiyo.
Salum Machaku wa Kilimanjaro Stas akiwa peke yake katika eneo la tukio na kupiga boooonge la shuti ambalo lilikwenda nje,huku golikipa wa Burundi akilisindikiza kwa macho.
Nyanda wa Burundi Niyonkuru Vladimir akiwapanga wachezaji wake wakati faulo iliyokuwa ikipigwa kuelekea langoni kwake.
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakifuraki kwa pamoja mara baada ya kupatikana kwa bao la pili lililofungwa na Nurdin Bakari.mabao hayo ndio yaliyoipelekea Kilimanjaro Stars kufuzu kuingia robo fainali ya mashindano Tusker Challenge Cup.
Washabiki wakishangilia bao la pili la Kilimanjaro Stars dhidi ya Burundi katika Uwanja wa Taifa jioni ya jana.
Habari na Picha Kwa HIsani Ya Michuzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)