Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya Kilimanjaro stars,Mrisho Ngassa akionyesha umahiri wake mbele ya beki wa timu ya taifa ya Somalia katika mchezo uliopigwa jana ndani ya uwanja wa Taifa jijini.Kilimanjaro stars iliweza kuibuka kidedea kwa kuichapa timu ya Somalia mabao 3-0. Jana uwanja ulijaa kwani kulikuwa hakuna kiingilio
Kiungo wa kati wa Kilimanjaro Stars,Henry Joseph akipena misuli na mchezaji wa timu ya Somalia katika mechi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliani wa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars,Nurdin Bakari akipachika bao la tatu dhidi ya Somalia mara baada ya kupata krosi maridadi kabisa kutoka kwa Mrisho Ngasaa.hadi mwisho wa mchezo Kilimanjaro stars 3-0 dhidi ya Somalia.
Nyanda wa Somalia akifanyiwa msaada wa kuvishwa jezi mara baada ya kufanyiwa matibabu na mmoja wa matabibu waliokuwepo uwanjani hapo.
Washabiki waliofurika katika uwanja wa Taifa Jana wakishangilia mara baada ya kupatikana kwa bao la tatu la timu ya taifa ya Kilimanjaro stars
Picha na Habari Kwa Hisani Ya Michuzi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)