Pichani Ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Nchini Mheshimiwa Lazaro Nyalandu(wa pili kulia) akiwa na na John Ndunguru wakati wa uzinduzi wa ndege za kampuni hiyo leo asubuhi.
Pichani Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu(kushoto)akizindua rasmi safari za ndege za Bold Air Leo kulia ni John Ndunguru
----
Watanzania wametakiwa kuacha kuogopa usafiri wa ndege kw akuwa zaidi ya jkuwa wa haraka lakini ni salama kuliko usafiri wa aina nyingine.
Akizindua Kampuni ya Ndege ya Bold Air leo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, LAzaro Nyalandu alisema wakati wa sasa usafiri huo iunatakiwa uwe wa kila mtu na si anasa kama watu wengi wanavyodhani.
"Kuna watu wanaogopa ndege kuna badghi ya waheshimiwa wata tukiwa Dodoma ukimwambia kuna ndege atakwambia 'Hapana ntadrive tutakutana Dar'
Bold Air ni kampuni inayomilikiwa na kijana wa kitanzania aishie Marekani, John Nduguru ambaye ameanza kwa ndege mbili ambazo zitakuwa zikienda sehemu mbalimbali nchini.
Nyalandu aliwataka watanzania zaidi walioko nje ya nchi kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ili kuleta ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi.
Alisema serikali imeweka mazingira mazuri na taarifa nzuri kupitia kutuo cha Uwekezaji (TIC) lakini wengi wamekuwa hawafuatilii na kuendelea kulaumu nchi haina mazingira mazuri kwa wawekezaji wazawa.
"TIC si kwajili ya wageni tu bali wawekezaji wa aina zote wanahudumiwa< nadhani watanzania zaidi watakuja kuwekeza nyumbani".
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)