WANZANZIBAR UINGEREZA WAMPONGEZA MAALIM SEIF - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANZANZIBAR UINGEREZA WAMPONGEZA MAALIM SEIF

Maalim Seif Shariff Hamad
------------
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jumuiya ya Zanzibar For Democracy inachukua nafasi hii ili kumpongeza Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad

(a) kwa busara, na hekima alizotumia kuunasihi umma wa kizanzibari kuondoka kwa usalama na utulivu huko Bwawani ili kuepusha na kuzuwia maafa na matatizo ambayo yangeweza kuvikumba visiwa vyetu;

b) kwa kuyakubali matokeo yaliyotolewa, kukubali huko kumedhihirisha uungwana na ustaraabu wake kwa lengo la kuvinusuru vizazi vijavyo ili viepukane na mizozo isioisha na kuondoa kabisa matatizo ya kiutendaji katika tume ya uchaguzi ya Zanzibar katika chaguzi zijazo na

(c) kwa hotuba yake aliyoitoa baada ya kutangazwa matokeo, hotuba hiyo imewafariji sana wazanzibari na wale wenye kuitakia mema Zanzibar na imekuwa ni pigo kubwa kwa maadui wa nchi yetu.Sisi tunayatafsiri mambo hayo kuwa ni vielelezo thabiti vyenye kuthibitisha ujasiri, umahiri, uadilifu na utendaji wake wa kiwango cha juu katika siasa za nchi yetu.

Tunatarajia kuwa viongozi wa Zanzibar mpya watajifunza na kufuata nyayo za Maalim Seif kuweka maslahi ya nchi mbele.Ni matumaini yetu kuwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo inatarajiwa kuanza kazi itawaunganisha wazanzibari bila ya kujali itikadi zao za kisiasa ili kufikia kuwa na Zanzibar moja; Taifa moja na Mustakbali mmoja.

"MUNGU IBARIKI ZANZIBAR"
Ahsante.

(Abdulla A. Abdulla),
KATIBU,
ZANZIBAR FOR DEMOCRACY(U.K.).
( 00447853180339)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages