JK AMTEUA JAJI FREDERICK WEREMA KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JK AMTEUA JAJI FREDERICK WEREMA KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Rais Jakaya Kikwete amteua tena Jaji Frederick Mwita Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Jaji Frederick Mwita Werema
-----------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Frederick Mwita Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia leo,Jumamosi, Novemba 6, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Phillemon Luhanjo inasema kuwa Jaji Werema ataapishwa saa 11 jioni leo katika shughuli itakayofanyika Ikulu.

Kabla ya uteuzi wake,Jaji Werema alikuwa anashikilia nafasi hiyo hiyo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Hivyo,anaendelea na wadhifa huo.

Rais Kikwete amefanya uteuzi huo saa chache baada ya kuwa ameapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha miaka mitano katika sherehe iliyofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Saalam.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages