TUME YA UCHAGUZI YAHAIRISHA UCHAGUZI BAADHI YA MAJIMBO NA KATA NCHINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TUME YA UCHAGUZI YAHAIRISHA UCHAGUZI BAADHI YA MAJIMBO NA KATA NCHINI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC ) Yahairisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata
Rajabu R. Kiravu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi
-----
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.

Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-
1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge,Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa anzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)
Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Madiwani utanaendelea kufanyika leo kama ilivyopangwa.

Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.
Kwa habari zaidi nenda


(Rajabu R. Kiravu)
Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages