KETE YA MWISHO MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KETE YA MWISHO MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA

TANZANIA leo inatupa kete yake ya mwisho na kusaka walau medali katika michuano ya 19 ya Jumuiya ya Madola inayomalizika kwenye Uwanja wa Jawaharlal-Nehru nchini India.

Tayari, imepoteza wanamichezo wake zaidi ya 20 na hivyo tumaini pekee kubaki kwa kwa wanariadha watano wa mbio ndefu, wanaume wakiongozwa na mshindi wa medali ya dhahabu wa michezo hiyo mjini Melbourne, Australia, Samson  Ramadhan.

Ramadhan na wenzake watatu watashiriki mbio za marathon za umbali wa kilometa 42 ambazo ndizo hitimisho la michezo hiyo na tumaini la mwisho la Tanzania kuambulia medali katika mashindano hayo.

Wanariadha  wengine , Shamba Kitin na Patrick Nyangero kwa upande wa wanaume huku kwa wanawake  akiwapo mzoefu, Restituta Joseph.

Akizungumza na Mwananchi jana, mkuu wa msafara wa Tanzania aliyeko India, Juliana Yasoda alisema kuwa wachezaji waliosalia wana morali kubwa ya kutetea nchi yao ili angalau iweze kuambaulia medali na si kurudi mikono mitupu.

"Wachezaji wetu wana uchungu wa kufanya vibaya, lakini pia waliosalia ambao wanafunga pazia la mashindano hayo kesho (leo), wana morali kubwa ya kuitetetea nchi yao na kutuondoa katika aibu ya kuwa wasindikizaji," alisema Yasoda.

Katika mashindano hayo yaliyofunguliwa rasmi Oktoba 3, Tanzania ilitupa karata yake katika mchezo wa kuogelea Oktoba 4 kwa mwogeleaji Mariam Foum aliyefanya vibaya akifuatiwa na wachezaji sita wa mpira wa meza ambao walishindwa kutamba siku hiyo mbele ya Ghana na kuishia kutolewa pia katika hatua za awali..

Pia, Tanzania ilipoteza wachezaji wake watatu  katika ngumi, wakifuatiwa na wenzao wa kuogelea  na hivyo kupoteza matumaini ya kuibuka na medali katika mashindano hayo.

Wachezaji hao ni Sunday Elias na Hashim Simon (ngumi), Khalid Rushaka (kuogelea) huko  Nasser Mafuru na Seleman Kidunda (ngumi)  walioanza kurejesha matumaini ya Watanzania yaliyokuwa yamepotea, nao wakishindwa kung'ara katika hatua ya mtoano na kuaga michezo hiyo.

Mwanariadha Damian Chopa,  mchezaji wa michezo ya walemavu,  Ignas Mtemve, mwogeleaji Magdalena Mosha, mabondia Haruna Swaga, Leonard Machichi na Revocatus Shomari pamoja na wanariadha  Marco Joseph,  Frank Martin na mwanariadha Barae Hera nao wakishindwa kung'ara

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages