Mwenyekiti
wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar, Balozi Seif
Ali Iddi, akiwapongeza makamanda wa vikosi vilivyoshiriki sherehe za
Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu wakati wa hafla ya kupongezana
iliyoandaliwa na Makamanda wa vikosi hivyo juzi usiku katika ukumbi wa
Hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Suleiman Iddi, akimtunza mtanashati Maryam Juma, katika wimbo wake wa kusifu
mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 49 kwenye tafrija ya kupongezana
makamanda baada ya kumaliza gwaride la shereh hizo Januari 12 mwaka huu.
Uzalendo ulimshinda Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud
Mohd, na kuamua kujumuika na Kikundi cha Utamaduni cha Diamond Modern
cha JKU kwenye tafrija ya makamanda kupongezana baada ya kumaliza
kuchapa gwaride uwanja wa amani.
Baadhi ya Makamanda
wa Vikosi vya ulinzi na usalama wakitafakari sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar mwaka huu wakiwa kwenye tafrija ya kupongeza Bwawani Mjini
Zanzibar.
Ilikuwa
ni siku ya furaha kwa makamanda wa Vikosi vya ulinzi na usalama
wakipongezana baada ya kazi nzito ya kuchapa gwaride Januari 12 mwaka
huu wa 2013. Picha Zote na Hassan wa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais,
Zanzibar
**************************
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujiandaa mapema na maandalizi
makubwa ya maadhimisho ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964
kutimia miaka 50 sawa na Nusu karne ambazo zitatarajiwa kuwa za
Kihistoria.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar ambae pia ni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa kauli hiyo wakati
wa tafrija maalum ya kupongezana na kuelewana kwa Maafisa wa Gwaride
iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif alisema ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali lazima kila
Mashirika, taasisi, Jamii na hata watu binafsi wanapaswa kuanza na
maandalizi mapema kwa lengo la kupata ufanisi unaokusudiwa.
Amesema
Serikali itaendelea kuunga mkono Vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwa
ndivyo vinavyonafasi kubwa ya kusherehesha vyema katika kilele cha
sherehe hizo za mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi
Seif alieleza kwamba Vikosi vya ulinzi na usalama vimefanya kazi mwaka
huu iliyopelekea kufurahisha na kupendeza miongoni mwa wananchi
walioshuhudia maadhimisho hayo.
“
Lazima niungame kwamba sherehe za mwaka huu zilikuwa za aina yake hata
baadhi ya wajumbe walioshuhudia maandalizi ya mwisho ya gwaride hilo
walipendekeza baadhi ya askari kutunzwa kutokana na ukakamavu
waliouonyesha”. Balozi Seif aliwapongeza maafandi hao kwa kazi nzito
walioifanya.
Alifahamisha kwamba Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yameleta faida kubwa kwa wananchi waliowengi na kuwafanya kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya kusherehekea sherehe hizo.
Akimkaribisha
Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe na maadhimisho ya Taifa Balozi Seif,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd
Aboud Mohd alisema majeshi ya ulinzi yameonyesha umahiri mkubwa katika
kuchapa gwaride.
Mh.
Aboud Alieleza kwamba Serikali inajivunia kazi kubwa inayotekelezwa na
majeshi ya ulinzi na usalama Nchini hasa wakati jamii inapokumbwa na
majanga na kupelekea maafa.
Mapema
Kamanda wa Brigedi 101 Zanzibar ambae ndie mkuu wa Gwaride hilo
Bridedia General Sharif Sheikh ameahidi kwamba Vikosi vya ulinzi na
usalama vitaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika kuona maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar kutimia miaka 50 yanafanikiwa vyema.
Brigedia
General Sharif Sheikh alieleza matumaini yake kwamba sherehe zijazo
zitakuwa za aina yake zinazotarajiwa kuwa za kistoria ndani ya Visiwa
vya Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.
Tafrija
ya Makamanda na maafisa hao wa Vikosi vya ulinzi na usalama imekuja
baada ya kazi kubwa na ngumu iliyofanywa ba Vikosi vyua ulinzi na
usalama katika kufanikisha gwaride la maadhimisho ya miaka 49 ya
Mapinduzi zilizochukuwa takriban siku 30.
Burdani
safi iliyokuwa ikitolewa na Kikundi cha Diamond Modern Taarab kutoka
Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar { JKU } ilianikiza ndani ya ukumbi huo
wa Bwawani hasa pale ulipoimbwa wimbo wa mafanikio ya Mapinduzi ya
Zanzibar kutimia Miaka 50 chini ya mwimbaji Mtanashati Maryam Juma.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/1/2013.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)