Mke
Wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa msaada vifaa vya kwa wawakilishi wa
kinduchi cha Mwambao Fishing Group katika bandari ya Lindi jana jioni.
Mke
Wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa msaada vifaa vya kwa wawakilishi wa
kinduchi cha Mwambao Fishing Group katika bandari ya Lindi jana jioni.
Mke
Wa Rais Mama Salma Kikwete na viongozi wengine pamoja na wawakilishi wa
kikundi cha Mwambao Fishing group waki vuta kamba kuzindua rasmi Boti
ya kikundi hicho jana wakati wa sherehe za makabidhiano yaliyofanyika
katika bandari ya Lindi jana jioni.
………………………………………………………
Na Freddy Maro,Lindi
Vijana kikundi cha Mwambao
Fishing Group wa Mji ya Lindi wamemshukuru mke Rais mama Salma Kikwete
baada ya kuwakabidhi Boti ya Uvuvi na vifa vyake katika hafla fupi
iliyofanyika katika bandari ya Lindi jana jioni.
Akisoma risala kwa niaba ya
wanachama wa kikundi hicho, Katibu Msadizi wa kikundi Bwana Jackson John
Mnenje alitoa ahadi ya kutunza boti hiyo na na kuvitumia kwa malengo
waliyojiwekea ikiwamo kununua boti nyingine baada ya mwaka mmoja
kutokana na faida itakayo tokana na biashara za uvuvi.
“Juhudi alizofanya Mama Salma,
zinaonyesha jinsi anavyoguswa na hali ngumu ya maisha ya Watanzania na
dhamira aliyonayo ya kutukwamua kutoka katika hali hii.Tunamshukuru
Mungu kwani leo sisi tumebahatika na kujiunga na Watanzania wengi
wanaofaidika na juhudi zake za kuboresha maisha ya Watanzania,”
wanakikundi hao walisema katika risala hiyo.
Kutokana na bei kubwa ya vifaa
hivyo, vijana hao wamesema kati ka risala yao kuwa, wasingeweza kamwe
kununua vifaa hivyo bila msaada huo uliotolewa na Mama Salma Kikwete na
kwamba utakuwa kichocheo kikubwa cha kukabiliana na na changamoto za
maisha zinazowakabili.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
Msaada huo,mke wa Rais Mama Salma Kikwete alisema msaada huo ni
utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010 na 2015 inayolenga kuwawezesha
wananchi kiuchumi na kuongeza kuwa ilani hiyo imetambua kuwa uvuvi ni
moja ya sekta za uchumi ambazo hazijapatiwa msukumo wa kutosha.
“Kuongeza ufanisi na tija na
kubadili maisha ya wavuvi ni moja ya Mapinduzi yanayolengwa katika ilani
ya CCM ya 2010 -2015 na mpango uliopo ni wa kuimarisha ushirika wa
makundi ya ujasiriamali ikiwa ni njia moja kubwa ya kuwawezesha
wananchi wa kawaida kumiliki na kuendesha uchumi,” alisema Mama Salma.
Mama Salma amesema kuwa Taasisi
anayoingoza ya Wanawake na Maendeleo WAMA itaendelea kuwasaidi wananchi
katika maeneo yao ya kujenga ushirika ulio imara na unaojitegemea
kiuchumi na unaoendeshwa na wao wenyewe katika misingi wa uwazi na
uwajibikaji.
Mama Kikwete amesema pia kuwa
WAMA inalo jukumu la kuhamasisha na kutoa msaada wa hali na mali kwa
wananchi na kuwawezesha kufikia malengo wali yojiwekea kwa kuwapatia
nyenzo na vifaa mbalimbali,lakini wajibu wa kujiendeleza na kujisimamia
unabakia wa watu wenyewe.
Mke wa Rais amewahimiza wanachama
wa Mwambao Fishing group kujenga mshikamano ili kikundi hicho kipate
utulivu utakao wapa fursa ya kupanga mipango ya kujenga na kuimarisha
kikundi na kufanya kazi kwa uwazi,kuaminiana na kupeana moyo.
Kikundi cha Mwambao Fishing Group
chanye wanachama 25 kilianzishwa mwaka huu katika manispaa ya Lindi
kutokana na ushari wa Mama Salma Kikwete aliyewashaur i vijana hao
kuunda kikundi na kubuni mradi wa maendeleo utakao wasaidia kuboresha
masiha yao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)