MBUNGE
wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ametoboa siri kuhusu usafiri wa treni ya
masafa mafupi jijini Dar es Salaam, akisema kuwa unaingizia hasara serikali
kiasi cha sh milioni 10 kila baada ya siku tano.
Kauli
hiyo ilitolewa jijini mwishoni mwa wiki na Mbunge huyo, wakati alipokuwa kwenye
ziara ya kichama katika Kata ya Saranga na Kimara.
Mnyika
alisema pamoja Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe kujitapa kuwa huduma
hiyo inakubalika kwa wananchi, bado haina tija kwa serikali kutokana na hasara
hiyo, inayotokana na gharama za uwendeshaji kuwa kubwa.
Alisema
mipango ya uanzishwaji ya usafiri huo ilikuwa yaa kurupuka kwani haikuwa na
maandlizi ya kutosha haswa katika upande wa miuondombinu ambayo nayo ni sehemu
inayoingiza hasara.
“Ninazo
nyaraka zinazoonesha mpango mzima wa
usafiri huu, ambazo zinaonyesha kuwa bado haujaleta jitija ispokuwa
hasara”alisema Mnyika.
Katika
hatua nyingine alizungumzia mabilioni ya fedha yaliyofichwa nchini Uswis,
Mnyika alisema serikali haipaswi kusubiri wahusika watajwe, kwani watu hao
wanafahamika.
Alisema
kwani baadhi ya watu waliyofanya hivyo ni miongoni mwa mafisadi waliyotajwa
kwenye mkutano uliyofanyika Septemba 15, 2007 kwenye viwanja vya Mwembe Yanga,
Temeke.
Mnyika
aliitaka serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya Rais Kikwete, isifanye
mzaha kuhusu mabilioni hayo, bali ifanye uchunguzi wa kina na wa haraka
kisha iwakamate na kuwafikisha
mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi huo wakutorosha mabilioni hayo.
Aidha,
alitoa angalizo kuwa endapo serikali hiyo ya CCM itashindwa kufanya hivyo basi
atalizimika kupasua bomu kwa kuwataja wahusika katika bunge lijalo.
Akizungumzia
kuhusu
kazi za chama, Mnyika alisema kuwa alifanya mikutano 10 kwenye matawi
ya kata hizo, ambapo miongoni mwakazi hizo ilikuwa ni kutoa
taarifa za utendaji wake wakazi katika kupigania kero zinazo wakabili
wananchi
wa jimbo hilo.
Pia
alizindua vikundi vya wajasiriamali ikiwemo Umoja wa Wanawake Mavurunza Kimaara
(Women Group), ambapo katika uzinduzi huo aliendesha harambee kwa ajili ya
kutunisha mfuko wa umoja huo.
Katika
harambee hiyo, Mnyika alichangia sh milioni 1, huku Wabunge wa Viti Maalumu
Naomi Kaihula na Joyce Limo wakichangia sh 500,000 kila mmoja huku jumla ya sh
milioni 3.8 zikipatikana katika harambee hiyo.
Naye
Mwenyekiti wa Umoja huo,Blandina Mrutu aliwashukuru viongozi hao, na kuahidi
kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa na umoja huo wenye
wanachama 15.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)