TASWIRA YA MAANDAMANO YA WAISLAM KUISHINIKIZA SERIKALI KUWAACHIA WENZAO WALIOKAMATWA KUTOKANA NA KUGOMA KUHESABIWA. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TASWIRA YA MAANDAMANO YA WAISLAM KUISHINIKIZA SERIKALI KUWAACHIA WENZAO WALIOKAMATWA KUTOKANA NA KUGOMA KUHESABIWA.


Mmoja wa viongoi wa maandamano hayo jina lake halijaweza kupatikana kwa haraka akiwahimiza waislam wenzake kuto kukata tamaa moaka kieleweke. Hapa wakiwa mbele ya jengo la wizara ya Mambo ya ndani kama linavyoonekana kwa mbele
Wakina mama wa kiislam nao hawakuwa nyuma katika maandamano hayo wakishinikiza waislam wenzao waliokamatwa kwa sababu ya kugoma kuhesabiwa watolewe, mpaka hivi sasa tunaingia mitamboni bado waandamanaji hao wapo katika jengo hilo la Wizara ya mambo ya ndani.
Wanahabari nao hawakua nyuma katika kupata picha za tukio hilo
Kwa juu kwenye ghorofa ni wafanyakazi wa Benk ya Exim iliyo karibu na Wizara hiyo wakiwa hawajui la kufanya huku wengi wao wakihofu kama mabomu ya machozi yakianza kupigwa watajisalimisha wapi, huku waislam kama unavyowaona kwa chini wakiwa wanaimba nyimbo mbali mbali za kuhamasishana kama iivyozoeleka kwa usemi wa kiimani yao "TAKHBIIRRR!!!!"
Hapa wakiwa wanaelekea kwenye wizara ya mambo ya Ndani. Tukio hilo limetokea muda mfupi uliopita. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ambayo imetolewa na jeshi la polisi kutokana na maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages