MIILI YA ASKARI WA JWTZ WALIFARIKI NCHINI SUDANI YAAGWA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MIILI YA ASKARI WA JWTZ WALIFARIKI NCHINI SUDANI YAAGWA LEO

 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya jeneza lenye mwili wa askari mmoja kati ya wa 3 wa jeshi hilo waliofariki kwa ajali ya maji  wakati wakivuka mto Lamada nchini Sudan, hivi karibuni wakati wakielekea kulinda amani chini ya jeshi la umoja wa Mataifa. Shughuli ya kuaga miili hiyo imefanyika leo mchana Lugalo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya jeneza lenye mwili wa askari mmoja kati ya wa 3 wa jeshi hilo waliofariki kwa ajali ya maji.
 Mkuu wa Majeshi nchini Devis Mwamunyange, akitoa  heshima za mwisho kwa miili ya marehemu.
 Katibu mkuu wizara ya ulinzi  akitoa  heshima za mwisho kwa miili ya marehemu.
Mkuu wa Majeshi nchini, Devis Mwamunyange, akimfariji mke wa mmoja wa askari waliofariki Bi, Fatuma Chunguile.
Askari wa JWTZ wakipakia moja ya jeneza lenye mwili wa marehemu katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea mikoani kwa ajili ya Maziko. Picha na JWTZ

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages