Mgeni
rasmi katika mashindano ya kuwania kombe Haniu Cup, ambaye pia ni
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akifuatilia
fainali hizo, kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Tongoni Mohammed
Mwinyihaji (CUF).
Mgeni
rasmi ambaye ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF),
akikabidhi zawadi ya kikombe cha ushindi kwa Nahodha wa timu ya Chuda
FC Ibrahimu Bodwe, baada ya timu yake kuibuka kidedea katika michuano ya
Haniu Cup, katikati ni Mratibu wa Mashindano hayo Mohammed Haniu.
Mashabiki
wa timu ya Chuda FC yakishangilia kwa ushindi walioupata dhidi ya timu
ya Jiwe FC baada ya kumalizika kwa fainali ya michunoa ya Haniu Cup
Jijini Tanga.
Na Mwandishi wetu, Tanga
HATIMAYE
timu ya Chuda FC ya Chumbageni Jijini Tanga, imetwaa ubingwa wa
mashindano ya Haniu Cup, kwa kuichapa kwa mikwaju ya penati timu ya Jiwe
FC yenye maskani yake Tanga Sisi.
Fainali
hizo ambazo zilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga, zilikuwa
za aina yake ambapo hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo
ziliweza kutoka sare ya bao 1-1.
Chuda,
ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuibuka na
ushindi wa mikwaju ya penati 4 kwa 1 hali iliyowafanya mashabiki wa timu
hiyo kutoka na shangwe uwanjani.
Akizungumza
katika mashindano hayo kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), alisema ni
muhimu kwa mkoa huo kuwa na kiwanja mbacho kitakuwa ni mahususi kwa
ajili ya kuibua vipaji wa soka mkoani humo.
“Mimi
kama Mbunge wetu wa Viti maalum na diwani wenu nina wajibu wa kusimamia
kwa karibu shughuliza maendeleo ikiwemo kunua soka katika mkoa wetu huu
wa Tanga. Mkoa huu ni chimbuko la michezo nchini na katika hili
nitahakikisha ninawasilisha hoja katika kikao cha Jiji ili kuweza
kijengwe kiwanja maalum ambacho.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)