Benki ya NMB imewafikia wanafunzi
45,000 wa shule za msingi katika mpango wake wa kukuza uelewa wa mswala
ya kifedha uitwao NMB Financial Fitness.
Mpango huo ulionanzishwa mwezi Mei
mwaka huu, una lengo la kuwahamasisha wanafunzi kujiwekea akiba kwa
kutumia huduma za kibenki wanapokua wakubwa.
Meneja wa NMB kanda ya Kusini,
Thomas Kilongo alisema katika taarifa yake kwamba, mpango huo
umeshawafikia wanafunzi 1,800 wa mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara katika
kampeni ya utoaji elimu iliyoanza wiki iliyopita.
Kilongo aliendelea kusema,
“wanafunzi hawa wamefundishwa namna ya kutunza fedha ikiwa ni
maandalizi ya kujiwekea akiba wakiwa wakubwa. Ili kufanikisha ndoto
zao , maandalizi yanatakiwa kuanza sasa na NMB inatoa mwanga wa namna ya
kufikia malengo yao,”
Wanafunzi waliopatiwa mafunzo hayo walionyesha hamasa ya kutaka kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu benki.
Akizungumza katika utambulisho
huo, mwanafunzi wa shule ya Liwale iliyopo mkoani Lindi Idrissa Ndumbaro
aliishukuru benki ya NMB kwa elimu hiyo ambayo baadae itamwezesha kuwa
na uelewa wa matumizi mazuri ya fedha pamoja na kujiwekea akiba .
Nae mwanafunzi Anna Daudi wa Shule
ya Msingi Ligula alisema, alifurahishwa na vitabu vya watoto NMB
Financial Fitness vinavyofundisha hadidhi juu ya kupanga matumizi ya
fedha na mengine mengi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)