Waziri Mkuu Pinda (kulia) akipeana mikono na Mhe. Sitta. Katikati yao ni Mhe. William Lukuvi. |
AKABIDHI KITI CHAKE BUNGENI KWA SAMWEL SITTA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na baba yake, imefahamika.
Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista
Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha
asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.
Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda
hatakuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba wa baba yake.
Akaongeza kuwa kwa sababu ya msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika
Mashariki, Mhe. Samwel Sitta kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia
leo (Julai 10) hadi Julai 15.Source: Strika Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)