Mkuu
wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala amefungua mafunzo ya mgambo
katika Kata ya Mnyambe Wilayani Newala, mkoani Mtwara jana
--
Akihutubia
wana mafunzo ya mgambo katika Kata hiyo ya Mnyambe, Mkuu wa Wilaya hiyo
amewaasa na kuwafafanulia wana mafunzo kwamba, mafunzo hayo ya mgambo
yapo kwa mjibu wa sheria namba 147 ya mwaka 1977 na kwa mjibu wa sheria
inayounda jeshi la Wananchi (JWTZ) ya mwaka 1966 na hivyo wapuuze
upotoshwaji unaotolewa na baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakieneza
uvumi kwamba mgambo haupo kwa mujibu wa sheria.
Aidha
Magala amesema kushiriki mafunzo ya Mgambo si lazima bali ni hiari ya
mtu mwenye kujitokeza na kujiandikisha ili kuwa wakakamavu na kupata
walinzi wazuri wa amani katika jamii.
"Mgambo
ni jeshi la akiba linaloundwa na raia wazalendo ambao wako tayari
kufanya kazi mbalimbali zinazofanywa na majeshi mengine kama kuokoa
maisha na mali za wananchi wakati wa maafa," alisema Magala.
Pia
DC Magala amewataka wana mafunzo ya mgambo kuwa mstari wa mbele na kuwa
mfano katika kutekeleza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za nchi
kwa kuwa na nidhamu kama wanajeshi wengine mara watakapomaliza mafunzo
hayo.
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya amewaambia faida zingine watakazopata mara baada ya
kumaliza mafunzo ya mgambo ni pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi
kupitia mpango wa ulinzi shilikishi/Polisi jamii katika maeneo
mbalimbali mijini na vijijini, kupewa kipaumbele pale majeshi yetu
yanapotaka kuajiri, na kupata ajira katika makapuni ya ulinzi:
"Serikali
imeyaagiza makampuni yote ya ulinzi kutumia wananchi waliopitia mafunzo
ya majeshi mbalimbali na mgambo lakini pia majeshi yote yameelekezwa
kuwapa kipaumbele waliopitia mafunzo ya mgambo wakati wa ajira zao,”
alisema Magala
Baada ya kufungua mafunzo ya mgambo Mkuu wa Wilaya ya Newala ametembelea shule ya Sekondari ya Mnyambe na kuikagua.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)