JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
Kufuatana na kifungu nambari 41 cha Sheria ya
Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010, Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania inapenda kufahamisha umma kwamba orodha ya Misimbo ya Posta au
‘postikodi’ za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechapishwa kupitia Gazeti ya
Serikali Notisi nambari 220 ya tarehe 22 Juni 2012.
Msimbo wa posta (Postikodi) ni mkusanyiko
wa tarakimu inayotambulisha eneo la usambazaji wa barua na kwa Tanzania eneo
linalotambulishwa ni Kata kwa Tanzania Bara na Wadi kwa Zanzibar. Kazi hii ya kitaalamu ya kugawa misimbo ya posta imefanyika baada ya
utafiti wa muda mrefu ambao umehusisha watalaamu mbalimbali. Ili kuufahamu
mfumo wa Msimbo wa Posta wa Tanzania, vigezo vifuatavyo vimetumika kama
ilivyofafanuliwa hapa chini.
1.
Ufafanuzi wa mfumo wa msimbo wa posta
Mfumo
wa msimbo wa posta wa Tanzania utaundwa na tarakimu tano
(5) ambazo zinatafisiriwa kama ifuatavyo:
Muundo wa Msimbo wa Posta
|
Maelezo
|
X X X X X
|
Tarakimu
5 (Mfumo wa Tarakimu za Msimbo wa Posta)
|
X - - - -
|
Tarakimu
ya kwanza = Kanda (1 – 7 tazama (a)
hapa chini)
|
X X -
- -
|
Tarakimu
mbili za kwanza = Mkoa
|
X X X - -
|
Tarakimu
tatu za kwanza = Wilaya
|
X X X X X
|
Tarakimu
zote tano = Kata/Wadi (Eneo la usambazaji)
|
Tarakimu
zote tano = Ofisi ya posta / mteja mkubwa / Eneo maarufu /Misimbo ya posta ya
shughuli maalumu.
|
(a) Tanzania imegawanywa katika kanda 6 na Zanzibar kama ifuatavyo;
1 - Dar es Salaam
2 - Kaskazini
3 - Ziwa
4 - Kati
5 – Nyanda za Juu Kusini
6 – Pwani
7 – Zanzibar
KANDA ZA
MISIMBO YA POSTA
(b) Tarakimu ya kwanza na ya pili ya msimbo wa
posta (kwa pamoja) inawakilisha mkoa katika Tanzania
(c) Tarakimu ya kwanza, ya pili na ya tatu (kwa pamoja) inawakilisha Wilaya
au Eneo la kati la Biashara katika Wilaya
(d) Tarakimu ya kwanza hadi ya tano ya msimbo wa posta inawakilisha Kata,
Wadi, Watumiaji wakubwa wa posta, Vitu maarufu na Shughuli maalumu
MIFANO YA MISIMBO YA POSTA;
11707: Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
23101: ICC, Arusha
33106: Kirumba, Mwanza
41105: Makole, Dodoma
57103: Mfaranyaki, Songea
63219: Msanga Mkuu, Mtwara
73104: Mkokotoni, Unguja
74209: Wawi, Chake Chake
2. Vigezo
vilivyotumika kugawa misimbo ya posta (postikodi)
|
Kigezo
|
Maelezo
|
1
|
Eneo la Utawala
|
Kata au Wadi imechaguliwa kuwa eneo la chini la usambazaji.
|
2
|
Ofisi za Posta
|
Kila Ofisi ya Posta itakuwa na msimbo wa posta. Mteja mwenye S.L.B
katika Posta fulani atatumia Msimbo wa posta (postikodi) ya Posta ile.
|
3
|
Watumaji wa barua wakubwa
|
Watumaji wa barua wakubwa kama Wizara za Serikali, Taasisi za Umma, Taasisi
za Udhibiti, Makampuni, Taasisi za Kimataifa, Taasisi zisizo za kiserikali
zitapewa msimbo maalumu wa posta.
|
4
|
Vitu maarufu
|
Eneo au umbo la kitu ambacho kimehifadhiwa kwa sababu ya kuhifadhi
historia litapewa msimbo maalumu wa posta.
|
5
|
Matukio au shughuli maalumu
(Kwa muda)
|
Kutakuwa na misimbo ya posta ambayo itahifadhiwa kwa ajili ya
kugawanywa endapo kutakuwa na shughuli maalumu katika nchi.
|
3. Anuani mpya zitawezesha ufikishwaji
majumbani barua na vifurushi. Kwa mfano anwani kamili inatolewa hapa chini:
Amos Mbawala
20 Barabara ya Mashele
23101 ARUSHA
2 – Kanda - Kasikazini
23 -
Mkoa - Arusha
231 – Wilaya - Arusha
23101 –Kata - Sekei
Orodha ya ‘Postikodi’
imechapishwa kwa ajili ya maeneo ya usambazaji ikijumuisha Mikoa, Wilaya na
Kata kama ilivyoainishwa 1 na 2 hapo juu. Orodha ya misimbo ya posta
(postikodi) itatolewa kwa ajili ya vigezo vingine vilivyooneshwa 3-5 hapo juu.
Umoja wa Posta
Duniani ambacho ni chombo cha Umoja wa Mataifa chenye wajibu wa kuendeleza
sekta ya posta katika nchi wanachama, utaarifiwa rasmi ambapo utawafahamisha
wadau wakuu wote duniani kuhusiana na matumizi ya mfumo mpya katika Tanzania.
Imetolewa:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
29
June 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)